Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka huu imetunukiwa kundi la kimataifa linalopigania kupigwa marufuku kwa silaha za nyuklia duniani.
Kamani ya Nobel nchini Norway imesema kundi hilo limekuwa shirika kuu la kiraia linaloongoza juhudi za kupigwa marufuku kwa silaha hizo chini ya sheria za kimataifa.
Kamati hiyo, inayoamua mshindi wa tuzo hiyo, imezihimiza nchi zenye silaha za nyuklia kuanzisha mazungumzo kuhusu kumaliza silaha hizo polepole.
Mwaka uliopita, Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ndiye aliyeshinda tuzo hiyo kwa sababu ya juhudi zake za kusitisha vita nchini humo kwa kufanikisha mkataba wa kusitisha vita na waasi wa Farc nchini humo.