Lawrence Masha Ampa Ushauri Rai Magufuli Sakata la Lissu

Masha amesema hayo akiwa kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na wanahabari, leo mchana na kusema kwamba  kwa sasa Watanzania wana hofu pamoja na hisia tofauti juu ya usalama wao hivyo ni vyema kukubali vyombo vya nje kufanya uchunguzi ili kupunguza hisia hizo.

"Kuomba msaada siyo fedheha. Msaada siyo jambo geni, kwa uzoefu wangu nilipokuwa Waziri  askari wengi walikuwa wanafanya 'training' nje naamini hata mpaka sasa. Tunapoomba msaada siyo kwamba haina uwezo bali inasaidia kuondoa hofu kwa wananchi. Ninachokuomba Rais waagize makamanda wako kuomba msaada ili Watanzania wasiishi kwa hofu" Masha.

Ameongeza kwa kusema kwamba "Tusikatae misaada, kwani hakuna aliyesema askari wa Watanzania siyo waadilifu japo wachache siyo. Siyo maisha yetu kukuta watu wamekufa ufukweni hofu kwa Watanzania hatujaizoea.

Pamoja na hayo Mh. Masha amekiri wazi kumshangaa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba pamoja na Inspekta Jenerali wa Tanzania Simon Sirro kwa kukataa msada wa kutoka nje wa kiuchunguzi ili kusaidia kupunguza hisia na hofu kwa Watanzania kwani ndiyo kazi ya jeshi la polisi.

Hata hivyo ameongeza na kutoa rai kwa serikali kwamba matukio hayo hayaathiri Watanzania tu kwani hata mataifa ya nje wanajiuliza kuhusu usalama wa Tanzania.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nasikia ulikuwa muheshimiwa.
    Je sasa status yako Ni mshayri muu WA wapi?

    ReplyDelete
  2. Ni nyinyi chadema mlitaka tanzania isipewe misaada, leo yamewakuta mnaishauri serikali hiyohiyo ikaombe msaada.......kwa nani?? na kwa nini hasa?? MDOMO-ULIPONZA-KICHWA

    ReplyDelete
  3. Msaada wa nini wakati yeye katusaliti vitani. Ndio akome kuwasaliti wenzie

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad