Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) Goodless Lema amefunguka na kusema kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti ametangaza kuwa anadau kubwa la kuweza kununua madiwani wengine 20 pia anadau kubwa kwa ajili ya Mbunge Joshua Nassari.
Lema amesema kuwa kitendo alichofanya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti ni wazi amethibitisha kuwa hata madiwani wa awali ni kweli waliwanunua hivyo amewataka TAKUKURU kuchukua hatua kwa kauli anazotoa diwani huyo.
"DC ambaye alitoa rushwa amethibitisha mwenyewe kuwa alitoa rushwa na DC amesema bado anafungu kubwa kununua zaidi ya madiwani 20 na anasema anadau kubwa kwa ajili ya Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mhe. Nassari kwa hiyo kama Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU alikuwa anatafuta ushahidi basi DC mwenyewe ameshampa ushahidi lakini nina uhakika Mlowola hatachukua hatua yoyote dhidi ya DC kwa sababu DC huyu huu ujasiri alionao anajua unatoka wapi" alisema Godbless Lema
Lema anasema kwa hali ya kawaida kiongozi hawezi kutoa kauli kama hiyo kwenye jambo ambalo ni nyeti kama hilo la ununuzi wa madiwani na kiongozi huyo akaendelea kubaki madarakani mpaka sasa. Aidha Lema amesema kitendo alichokifanya Mnyeti ni dhihaka kubwa na dharau ya juu sana kwa Umma.
Kwani Lowasa alipohamia chadema kuna dau mlimpa?
ReplyDeleteamakweli 'KUNYA-ANYE-KUKU-AKINYA-BATA-KAHARISHA' hahahaha
HV mnyeti si rc au lema hujui
ReplyDelete