Mwenyekiti wa (CUF) anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa Lipumba amefunguka na kumsifia Rais John Pombe Magufuli kwa hatua mbalimbali anazochukua juu ya maliasili za nchi hii na kusema Rais amechukulia jambo hilo umuhimu.
Lipumba amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye hafla ya kupongezwa na kupewa vyeti kwa wajumbe walioshiriki kwenye kamati za uchunguzi wa madini alimaarufu kama makinikia.
"Kwa niaba ya vyama vya siasa nchini naomba kumpongeza Rais kwa juhudi alizofanya kwenye suala hili la madini, sisi viongozi wa upinzani kwa muda mrefu, kwa miaka mingi tumekuwa tukipiga kelele sana kuhusu mikataba ya madini na maliasili za nchi hii, itakuwa ajabu sana sisi tuliokuwa mstari wa mbele kupiga kelele kwamba tunaibiwa kubeza juhudu unazofanya sasa" alisema Lipumba
Aidha Lipumba ametoa ushauri kwa serikali kuwa watu ambao wanatakiwa kuingia kwenye bodi za kampuni mpya wa madini kuwa wanapaswa kuwa wazalendo kweli na kwenda kusimamia maliasili za nchi na kudai bila kufanya hivyo tutalizwa tena.
"Watanzania wanatakiwa kushiriki kwenye kampuni hizo ambazo zitakuwa na uwazi na faidi inayopatikana inapaswa kuwa nusu kwa nusu, lazima Watanzania watakaoshiriki katika kampuni wanatakiwa kuwa wazalendo kulinda masilahi ya taifa, kwa sababu tumekubaliana kugawana nusu kwa nusu lakini mkajikuta wametangaza faidi ya asilimia 0 hivyo hiyo 0 ukigawanya kwa mbili unapata 0 palepale, kwa hiyo watakaoingia ndani ya kampuni wahakikishe utaratibu wa kudanganywa haupati nafasi" alisema Lipumba
Lipumba amesema kuwa wao watamuunga mkono Rais John Pombe Magufuli na kusema kuwa katika hutua hii wanatanguliza maslahi ya Tanzania kwanza na maslahi ya Vyama Vya Siasa yatafuata baadaye.
Wenzako wamemfuata ili kumuunga mkono
ReplyDelete