Lundenga Aitolea Povu Serikali Asema 'Kufungia Sanaa au Wasanii Kunadidimiza Sanaa Yetu'

Lundenga Aitolea Povu Serikali Asema 'Kufungia Sanaa au Wasanii Kunadidimiza Sanaa Yetu'
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waendeshaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga amefunguka na kutoa lawama kwa serikali kuhusu sakata la kufungia fungia wasanii na kazi za sanaa na kusema jambo hilo linadidimiza sanaa.

Ludenga amesema hayo leo alipokuwa akihojiwa kwenye Jukwaa la sanaa ambalo limeandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo leo limefanyika katika wa Taifa Dar es Salaam, na kusema kitendo cha serikali kufungia wasanii na kazi za sanaa kimekuwa kikwazo na kudidimiza sanaa nchini.

"Mimi leo nimekuja hapa hakuna ajenda maalum ila nikipata nafasi nitatoa yangu ya moyoni, suala la kufungia sanaa au wasanii huko si kuendeleza sanaa  bali ni kudidimiza sanaa yetu, ingependeza msanii anapofanya kosa fulani kuwe na faini fulani ambayo mtu analipa lakini siyo kumfungia, anapokiuka utaratibu au sheria kuwe na faini tu kama kwa wenzetu wa mpira wa miguu" alisema Ludenga

Ludenga anasema msanii anapofungiwa kwa wakati fulani anapokuja kurudi inamchukua muda na anakuwa anaanza upya katika sanaa jambo ambalo linarudisha nyuma sanaa na maendeleo ya sanaa kiujumla.

"Unapomfungia msanii kuja kuanza tena mpaka aje kusimama kama alivyokuwa wakati unamfungia inachukua muda na gharama zaidi hivyo unakuwa unadidimiza sana badala ya kuboresha, mfano sisi tumefungiwa mwaka 2014, na sababu za kufungiwa ni kutokana na makosa ya mawakala wetu, kumbuka wakati tunafungiwa tulikuwa na wadhaamini kabisa huku ni kurudishana nyuma" alisisitiza Ludenga.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad