Maandamano ya Nasa Nchini Kenya Yapigwa Marufuku Kenya

Maandamano ya Nasa Nchini Kenya Yapigwa Marufuku Kenya
Serikali ya Kenya imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika katika miji mitatu mikubwa ikiwamo jiji la Nairobi ikitaja kasoro zilizoonekana wakati wapinzani walipofanya maandamano hivi karibuni dhidi ya tume ya uchaguzi.

Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiangi amesema kutokana na wasiwasi wa uwezekano wa kujitokeza kwa vitendo vya uvunjifu wa amani Serikali imeamua kuyapiga marufuku maandamano ya aina yoyote yaliyopangwa kufanyika katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.

“Kutokana na ukweli kuwa uko uwezekano wa kujitokeza kwa uvunjifu wa amani, tunatangaza kuwa Serikali haitaruhusu kufanyika maandamano yoyote katika miji ya kibiashara ya Nairobi, Mombasa na Kisumu,” amesema waziri huyo.

Amesema taarifa ya zuio la kutofanyika kwa maandamano hayo pia limetumwa kwa mkuu wa jeshi la polisi.

Kumekuwa na taarifa kuwa muungano wa Nasa umepanga kufanya maandamano katika miji hiyo kwa lengo la kushinikiza tume ya uchaguzi kufanyiwa mabadiliko kabla ya uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26.

Waziri Matiangi amesema waandamanaji hao walionekana wakishambulia vituo vya polisi, maofisa wa polisi na kuwajeruhi  huku wakivuruga shughuli nyingine zilizokuwa zikiendelea wakati walipoandamana hivi karibuni.

Mgombea wa Nasa, Raila Odinga ametangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad