Pacha walioshikana kichwani Jaga na Kalia
Madaktari wa upasuaiji katika mji mkuu wa India Delhi wamefanikiwa kuwatenganisha wavulana pacha waliokuwa wameshikana katika kichwa.
Wavulana hao wa miaka miwili Jaga na Kalia walifanyiwa upasuaji uliochukua takriban saa 16 na sasa wako katika chumba wagonjwa mahututi ICU, kulingana na madaktari.
Kundi la madaktari 30 walifanya upasuaji huo katika taasisi ya matibabu na sayansi ya All India.
Wavulana hao walizaliwa wakiwa na wanatumia mishipa ya damu ya pamoja mbali na tishu za ubongo, hali isio ya kawaida ambayo hutokea mara moja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo Randeep Guleria aliambia vyombo vya habari vya India kwamba siku 18 zijazo zitakuwa muhimu ili kuthibitisha ufanisi wa uchaguzi huo.
Pacha hao wanaotoka katika kijiji cha mashariki cha jimbo la Orissa walikuwa wameshikana katika kichwa, hali inayoitwa 'craniopagus'.