Magufuli Huenda Akawa Rais wa Pili Kuenziwa Zaidi Baada ya Mwalimu

Ni wazi kuwa kila Rais mstaafu ameacha legacy yake, ambapo baadhi yao wanakumbukwa zaidi ya wengine. Hadi sasa naweza kusema hakuna Rais aliyeacha legacy nzuri inayoishi, na itakayoishi vizazi na vizazi kuzidi ile iliyoachwa na Mwalimu Nyerere. Licha ya kuwa utawala wa Mwalimu umekuwepo wakati wengi wetu tukiwa ama wadogo sana kuweza kupambanua mambo au tukiwa hatujazaliwa kabisa, lakini kwa nguvu ya historia nzuri aliyoiacha tumekuwa tukimzunguzia as if ndiye Rais tuliyefurahia sana utawala wake. Mwalimu amekuwa ni Benchmark ya utawala ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.

Lakini pia historia inatuambia kuwa Mwalimu huenda akawa ndiye Rais pekee aliyepitia magumu kuzidi Marais wote so far katika utawala wake. Yumkini hadi sasa akawa ndiye Rais wa kwanza kuchukiwa enzi za utawala wake kuzidi Marais wengine hadi kufikia hatua ya kutaka kupinduliwa mara kadhaa. Hali hiyo haijasikika hadi sasa kama kuna Rais yeyote aliyei-face wakati wa utawala wake, labda iwe imetokea na kuzimwa kwa siri kubwa sana. Naweza kusema kuwa nia na dhamira njema ya Mwalimu juu ya hatma ya nchi yetu ndivyo vinavyompa sifa kubwa kwa sasa, licha ya kuwa wakati wa utawala wake watu wengi hawakumwelewa na wengine kumuita dikteta.

Nikiangalia kwa upande mwingine, kwa kipindi kifupi ambacho Rais Magufuli ametawala, amekuwa ni “Talk Of The Day”. Ni Rais aliyepenya mioyoni mwa watu wengi sana, wadogo kwa wakubwa kwa kipindi kifupi kuzidi Marais wengi waliopita. Leo unaweza kumuuliza hata mtoto mdogo sana jina la Rais akakutajia, na pengine na mambo kadhaa kumhusu Rais huyo tofauti na ilivyokuwa kwa mihula kadhaa hapo awali. Ni ukweli usiopingika kuwa amepenya mioyoni mwa watu kwa namna tofauti, wapo wanaompenda sana na wale wanaomchukia pia kitu ambacho si kigeni kwani kimewatokea Marais wote waliopita.

Naweza kusema kuwa kumekuwa na tofauti kubwa ya kutafsiri dhamira au nia ya Rais JPM na hatma ya nchi yetu katika utawala wake. Kwa mtazamo wangu naona nia yake ni njema sana, pengine akitaka kutupeleka kule ambako Mwalimu Nyerere alipenda tuwepo. Kuwa katika nchi ambayo watu wote tunaifurahia, tunaheshimiana, tunathaminiana, na kunufaika kwa rasilimali zetu. Kuwa katika nchi ambayo mirija ya unyonyaji inazibwa na haki inatamalaki. Kwa kifupi ni kuwa katika nchi ya neema. Wale wasiompenda huenda ndio walikuwa wanufaika kwa njia zisizo halali, hivyo kuzibwa kwa mianya ya unyonyaji, rushwa n.k kunawafanya waishi kama mashetani.

Kwa kuwa Rais Magufuli amekuwa akionesha dhamira au nia yake hiyo wazi wazi, ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za makusudi na kwa haraka ili kuhakikisha kuwa malengo yake yanatimia, kuna uwezekano mkubwa JPM akawa ni Rais wa pili kuenziwa zaidi baada ya Mwalimu endapo Marais watakaomfuata hawatafanya vizuri sana zaidi yake.

Benmpo
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kweli kabisaa. tena wa kwanza kumuenzi atakuwa Bashite na shoga yake Le mutuz. mademu wa Jery muro.

    ReplyDelete
  2. Wewe anony 10:48.
    Inaelekea ni mkosefu WA Adabi na hukupata malezi bora...!!!!
    Matusi au lugha chafi SI hulka yetu Watanzania.
    Hata kama unachuki BASI kaa nazo na usiziweke ulivypfanya...mungu akusamehe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad