Mahakama hiyo ya juu iliamua kwamba matokeo ya uchaguzi yaliotangazwa katika maeneo bunge ni ya mwisho.
Katika uamuzi wa mwisho , majaji watano wa mahakama hiyo walisema kuwa kulikuwa na hitilafu kati ya matokeo ya fomu 34A na 34B, mwenyekiti anafaa kutangaza matokeo ya uchaguzi na kuwaachia mahakama swala hilo kuamua.
Majaji hao walisema kuwa bwana Chebukati ana wajibu wa kukagua matokeo hayo kama yalivyopeperushwa kwa njia ya kielektroniki.
Hatahivyo kila anapokumbana na hitilafu , anapaswa kuelezea vyama vilivyopo, wachunguzi wa uchaguzi na raia na kuwachia swala hilo mahakama ya uchaguzi.
Katika uamuzi uliosomwa na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu ,mahakama ilisema kuwa uwezo wa mwenyekiti kuchunguza matokeo sio agizo lililotolewa na mahakama bali ni sheria iliopo katika katiba na sheria za uchaguzi.
Katika kesi yake, tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC ilisema kuwa ombi hilo lilikuwa haliangazii uamuzi wa mahakama ya juu wa tarehe mosi mwezi Septemba.
Kamishna wa tume ya uchaguzi Kenya azuiwa Uwanja wa ndege
Tume ya uchaguzi Kenya yatetea uamuzi kuhusu tarehe ya uchaguzi mpya
Chama cha Kenyatta chapinga maafisa wapya wa uchaguzi Kenya
Tume hiyo iliongezea kwamba ombi hilo sio rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya rufaa inayojulikana kama Kesi ya Maina Kiai, ilioamuru kwamba matokeo yatakayotangazwa katika vituo vya kupigia kura ndio matokeo ya mwisho