Mahakama ya Afrika Kusini Yaamuru Rais Jacob Zuma Ashtakiwe

Mahakama ya Afrika Kusini Yaamuru Rais Jacob Zuma Ashtakiwe
Mahakama ya juu ya rufaa nchini Afrika Kusini imeamuru kwamba Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma lazima akabiliane na mashtaka ya rushwa, kugushi na kujihusisha na mtandao wa utakasishaji fedha.

Mahakama hiyo ilikubali uamuzi wa mahakama ya chini katika uamuzi wake ilioutoa mwaka uliopita, mahakama hiyo ikiwaamuru waendesha mashtaka wanawewza kuyarejesha mashitaka 783 ya rushwa inayohusiana na makubaliano ya kununua silaha ya mwaka 1999.

Mashtaka hayo yaliwekwa pembeni miaka minane iliyopita na kumuwezsha Zuma kuwania na kushinda urais wa nchi hiyo na kushinda. Rais Zuma mara zote amedai kuwa hana hatia na katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake inasema maamuzi hayo ya mahakama ya juu yanasikitisha lakini alitarajia hivyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad