Mahakamani:Shahidi wa Kwanza Seth Bosco Atoa Ushahidi wa Kifo cha Kanumba

Mahakamani:Shahidi wa Kwanza Seth Bosco Atoa Ushahidi wa Kifo cha Kanumba
Mahakama kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika imeanza kuisikiliza shauri la kesi ya jinai namba 125 ya mwaka 2012, Inayomkabili  Msanii Elizabethi Michael ya kumua msanii mwenzie Steven Kanumba bila kukusudia mbapo leo upande wa jamhuri ulikuwa na Mashahidi 2 na shahidi namba moja alikuwa ni Mdogo wake Steven Kanumba Aliyejitabulisha kama Seth Bosco, lakini shahidi wa pili aliomba udhuru wa kutofika leo.

Katika maelezo ya Shahidi Seth Bosco akiongozwa na wakili wa Jamhuri Faraja George ameieleza mahakama kuwa Kanumba ndiye aliye mfungulia mlango Lulu, na alipofika ndani baada ya muda kidogo yeye akiwa chumbani kwake alianza kusikia mvutano wa sauti ya Kanumba ikimwambia Lulu

"kwanini Unaongea na 'Boyfriend' wako mbele yangu?" Mabishano yalianzia kwenye korido, na baada ya kuingia chumbani zilianza kusikika kelele

Baada ya muda mfupi Lulu aliinita na kuniambia Kanumba ameanguka najaribu kumwagia maji naona haamki, nilipoingia chumbani nikweli nilikuta yuko chini akiwa ameegemea ukuta, nikamchukua nikamlaza chali na ndipo nilipoanza kumtafuta Daktari wake anayeitwa Paplas Kageiya, daktari alipofika alimfanyia 'Chek up' akasema ameshafariki, akashauri tumpeleke Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, niliendesha gari mpaka muhimbili, tulipofika muhimbili kwenye kitengo cha dharura walituambia tukatafute utaratibu wa kipolisi, wakati wao wanaandaa vibali vya kuruhusiwa apelekwe mochwari, Baada ya mahojiano ya Polisi katika kituo cha urafiki Ubungo, niliondoka na Askari kurudi nyumbani kwaajili ya uchunguzi, baada ya polisi kufika pale wakiwa chumbani wanaendelea na uchunguzi walikuta Panga chini ya kitanda" Alisema shahidi Seth Bosco

Baada ya ushahidi huo, mahakama imeahirisha shauri hilo hadi kesho Oktoba 20, 2017 kwaajili ya kuendelea kusikiliza mashidi wengine Wanne kutoka upande wa Jamhuri.

Upande wa mstakiwa unaongozwa na Wakili Msomi Peter Kibatala.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa kwa siku tatu mfulilizo, ingawa Jaji Rumanyika ameelekeza upande wa mstakiwa na Jamhuri kuona kama wnaweza kutumia hata siku mbili kuisikiliza na siku ya tatu ikatumika kuandika hukumu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad