Mambo Usiyopaswa Kusema Wakati wa Interview

Tumekuwa tukiambiwa kuwa usidanganye hata kidogo katika usahili wa kazi uliyoiomba. Ni kweli hupaswi kudanganya, kwa sababu utakapogundulika kuwa umedanganya utajiweka katika hatari ya kuikosa kazi unayoiomba.

Lakini siyo nyakati zote unapaswa kusema ukweli katika usahili wa kazi. Mambo mengine huwa ni ya kweli lakini yatakuharibia sifa yako na pengine utaikosa kazi unayoitafuta.

Hakuna mtu aliye tayari kuikosa kazi anayoiomba. Kila mmoja atafanya jitihada kuhakikisha kuwa anakuwa bora zaidi katika usahili na kuwazidi wengine.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo hata kama ni ya kweli hutakiwi kuyasema katika usahili wa kazi.

Usiandike kila kitu katika wasifu wako (CV)

Unapoenda katika usahili wa kazi, uasiandike kula jambo ulilowahi kulifanya katika wasifu wako (CV). Baadhi ya mambo yanaweza kumpa wasiwasi mwajiri wako. Hebu fikiri uliwahi kufanya kazi katika kampuni fulani, baada ya miezi miwili ukafukuzwa kazi kutokana na uzembe, ukiiweka hiyo kazi katika wasifu wako kisha muajiri akakuuliza kwa nini uliifanya kwa muda mfupi, utamjibu nini?

Usimsemee vibaya muajiri wako wa zamani

Jambo kubwa linalowafanya watu wengi kuacha kazi walizokuwa wakizifanya ni pamoja na mahusiano mabaya na waajiri wao. Unapoenda katika usahili wa kazi mpya, usimsemee vibaya muajiri wako wa awali hata kama hamkuwa na mahusiano mazuri. Eleza kuwa umejifunza mambo mengi kutoka kwake. Hii itakusaidia wewe na itamfanya muajiri wako mpya akufikirie mara mbili katika usahili huo.

Usieleze sababu iliyokufanya uache kazi uliyokuwa unaifanya awali

Ukweli ni kwamba watu wengi huacha kazi moja na kutafuta nyingine kwa sababu ya mambo kama vile, mahusiano mabaya na waajiri au wafanyakazi wenzao, ugumu wa kazi yenyewe, kiwango cha mshahara na mengine yanayofanana na hayo. Lakini wakati unafanyiwa usaili hakikisha hutaji mambo hayo kama ndiyo sababu iliyokufanya wewe kutafuta kazi nyingine. Badala yake eleza ni kwa kuwa hii ndiyo kazi unayoipenda na utaifanya vizuri zaidi kuliko ya awali.

Hakikisha mambo unayoyapendelea yanaendana na aina ya kazi uliyoiomba

Usitaje unapendelea kunywa bia, kwenda kustarehe na marafiki, kuangalia filamu, kuchati na mengine yanayofanana na hayo, vinginevyo unaomba kazi kaztika kampuni ya bia ama inayohusiana navyo. Badala yake taja mambo kama vile kusoma vitabu, kuhudhuria warsha mbalimbali, kujifunza n.k
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad