Maneno ya Lowasa Baada ya Nyarandu Kujiudhuru 'Tumelamba Dume'

Maneno ya Lowasa Baada ya Nyarandu Kujiudhuru 'Tumelamba Dume'
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua nyadhifa zote alizokuwa nazo CCM.
Akionyesha kuwa na furaha alipozungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”.
Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango.
Dakika chache tangu Nyalandu aombe kujiunga na Chadema, Lowassa alimkaribisha waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii huku akisema mwanasiasa huyo amechelewa kujiunga na upinzani.
“Mbona amechelewa? Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake,” alisema Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne.
“Nyalandu ni hazina, ni mbunge imara na ni mwanasiasa wa mfano,” alisema Lowassa, ambaye alijiunga na Chadema mwaka 2015 na kuwania urais kupitia muungano wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa).
Lowassa alimsifu Nyalandu kwa kuisaidia jamii na akatoa mfano jinsi alivyosaidia watoto watatu wa Shule ya Lucky Vincent waliokwenda kutibiwa Marekani baada ya kupata ajali ya basi iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja.
“Nyalandu ana contacts (anafaham watu wengi) nyingi na jumuiya ya kimataifa, ni bidhaa nzuri kuwanayo,” alisema Lowassa, ambaye katika uchaguzi wa urais alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 6,072,848 (asilimia 39.97) ikiwa ni rekodi ya kura nyingi kwa upinzani tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe mwaka 1992.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. lazima ahame kwani hakuna ulaji sasa hivi kote kumeminywa, Na wamewekwa pembeni kabisa Sasa wanatapatapa

    ReplyDelete
  2. mmelamba dume. ili mje msaidiane kufisadi tena, maanake huko nyuma wote mna story za wizi na ufisadi. Unafuraia ili mnawaza mkipata nchi Malambe vizuri aswaaa

    ReplyDelete
  3. What a joke!yani baada ya vyuma kubana ndio anatambua kuwa wananchi wanahitaji katiba mpya na kuwa kuna mgongano wa mihimili ya uongozi nchini? Really! Wakati ule akiwa anabembea akitafuna hela za walipa kodi hakuyaona hayo?

    ReplyDelete
  4. KUTOKA-CCM-KWENDA-CHADEMA-NI-SAWA, UKITOKA-CHADEMA-KWENDA-CCM-UMEHONGWA-AMAKWELI-KUNYA-ANYE-KUKU-AKINYA-BATA-KAHARISHA!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad