Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Nikki Haley, ameiambia Jamhuri ya kidemokrasi uya Congo kufanya uchaguzi uliocheleweshwa 2018.
Bi Haley alionya kuwa usaidizi wa Marekani kwa taifa hilo uko hatarini iwapo hatua hiyo haitatekelezwa.
''Uchaguzi lazima ufanyike 2018 la sivyo DR Congo isitarajie msaada wowote kutoka kwa Marekani na jamii ya kimataifa', aliripotiwa na chombo cha habari cha AFP akisema.
Alitoa matamshi hayo baada ya kukutana na Corneille Nangaa mkuu wa tume ya uchakuzi nchini humo.
Uchaguzi ulitarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2016, lakini tume hiyo ya uchaguzi ukauahairisha kufuatia ukosefu wa mipango na fedha.
Marekani imesema kuwa mbali na maswala mengine ya kutia wasiwasi ya usalama ni mgogoro unaeondelea katika jimbo la kati la Kasai.
Tume hiyo wiki mbili zilizopita ilitangaza kwamba tarahe ya karibu ambapo taifa hilo linaweza kuandaa uchaguzi ni mwezi Aprili 2019.
Maandamano ya upinzani yamefanyika katika maeneo mbali mbali nchini humo dhidi ya kuongezwa kwa muda wa kutawala wa rais Kabila.
Bwana Kabila alitarajiwa kuachia madaraka mnao mwezi Disemba 2016 lakini katika makubaliano yaliofikiwa na viongizi wa kanisa katholiki, ilikubalika kwamba ataondoka afisini mwisho wa 2017.