Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imesema inaheshimu lakini inajutia uamuzi wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, kujiondoa kwenye Uchaguzi mpya wa urais tarehe 26 mwezi huu.
Hata hivyo, Marekani imeendelea kusisitiza kuwa, itaendelea kushinikiza kuwepo kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.
Afisa wa juu katika Wizara hiyo ameliambia Gazeti la Daily Nation kuwa, pamoja na hilo Odinga anakaribishwa nchini Marekani.
Taarifa hii imekuja baada ya kuwepo kwa madai kuwa Odinga amenyimwa Visa ya kwenda Marekani.
Marekani imesema hakuna kinachomzuia Odinga kuja nchini Marekani wakati wowote anaotaka.
Kwa sasa Odinga yupo jijini London nchini Uingereza, anakotoa midhahara ya kisiasa na kukutana na viongozi mbalimbali