Agnes Gerald maarufu kama ‘Masogange’ amerudi tena kwenye headlines za Mahakamani tena leo October 12, 2017 ambapo hata hivyo, kesi yake ya kutumia dawa za kulevya imesogezwa mbele katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi November 14, 2017.
Masogange alitarajia kuanza kujitetea leo lakini Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alimuomba Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri aahirishe kesi hiyo hadi tarehe nyingine ambapo kutokana na ombi hilo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi November 14, 2017.
Masogange ataanza kujitetea baada ya Mahakama kumkuta na kesi ya kujibu kwa upande wa mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi watatu.
Masogange anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
Pia anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
Massogange Azidi Kukwama Mhakamani Kesi Yake Yasogezwa Mbele
0
October 12, 2017
Tags