Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria wa Umoja wa Mataifa umesitisha msaada wake wa kifedha kwa nchi ya Burundi.
Mfuko huo umetoa zaidi ya dola za Marekani milioni 275 kwa nchi hiyo katika kipindi cha miaka 14, na kueleza kuwa hatua ya kusimamisha msaada huo ni kutokana na matumizi mabaya ya fedha hizo.
Kwa mujibu wa barua ya mfuko huo kwa Waziri wa Afya wa Burundi, Josiane Nijimbere, pamoja na mambo mengine inatuhumu kuajiri kinyume cha sheria, maamuzi ya kufukuza wafanyakazi kiholela, kuingiliwa kwa usimamizi, na gharama za magari.