Ikiwa ni miaka miwili imepita tangu aliyekuwa Mbunge wa Ludewa Deo Haule Filikunjombe afariki dunia, mke wa wake Sarah Habiba amesema Tanzania ina pengo kubwa kwa kumpoteza Deo.
Kwenye ukurasa wake wa instagram, Sarah Habiba ameandika ujumbe huo, wakiadhimisha miaka miwili ya kifo chake kwa kufanya ibada takatifu.
"Mume wangu leo umefikisha miaka miwili tangu upatwe na mauti, kiukweli umeacha pengo kubwa kwa watanzania, jamii na familia kiujumla, watoto wako wanakumiss sana, mimi mkeo, Mungu akulaze mahala pema peponi mpenzi wangu, ntakukumbuka daima mpenzi", ameandika Sarah Habiba.
Deo Filikunjombe alifariki )ctoba 15, 2015 kwa ajali ya helkopta akitokea Dar es salaam kwenda Ludewa, na kuanguka kwenye msitu wa mbuga ya Selous, akiwa na rubani wake William Silaa ambaye ni baba mzazi wa Jerry Silaa, na msaidizi wa Deo Filikunjombe, Bwana Mkwera.
Deo Filikunjombe atakumbukwa kwa uchapa kazi wake na juhudi alizozionyesha kwenye kamati ya Bunge kuibua sakata la Escrow akiwa na wabunge wengine, akiwemo rafiki yake wa karibu mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.