Mke wa Dr Slaa Atoboa Siri Kubwa Kuhusu Afya ya Marehemu Kanumba

KESI inayomkabili muigizaji, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ya kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake Steven Kanumba, imeendelea kusikilzwa  leo Jumatano, Oktoba 25 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Leo ilikuwa ni siku ya kusomwa kwa maelezo ya ushahidi ulioandikwa na mke wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Slaa, Josephine Mshumbusi,  ambaye pia alikuwa daktari wa marehemu Kanumba. Mshumbusi alishindwa kufika mahakamani jana kutokana na kuwa nchini Canada.
Melezo ya Mshumbusi yamesomwa mahakamani hapo na Askari wa Kituo cha Polisi, Oyster Bay,  Detective Sajenti Nyangea ambaye ndiye alisaini maelezo ya ushahidi huo.

Akisoma maelezo hayo, Sajenti Nyangea amesema; “Mmoja ya wateja wangu, marehemu, Steven Kanumba kwa mara ya kwanza alikuja kwangu mwaka 2011 kwa ajili ya kutoa sumu mwilini. Marehemu alikuwa na matatizo ya damu, upungufu wa hewa kwenye ubongo na alikuwa anasikia maumivu katika ubongo na akili kuchoka,” alisoma Sajenti Nyangea.

Aidha Jaji ambaye anasikiliza kesi hiyo amesema kwa kuwa Sajenti Nengea hawezi kuulizwa swali lolote kwa kuwa yeye alikuwa anasoma ushahidi ambao uliandikwa na mtu mwingine.
Jaji huyo ameongeza kuwa kesho siku ya Alhamisi wazee wa baraza watakaa na kujadili kama Lulu ana hatia katika kesi hiyo inayomkabili au la.

Global

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad