Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati Akutana na Raila Odinga

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati Akutana na Raila Odinga
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati akutana na mgombea urais wa upinzani Raila Odinga.
Bw Chebukati amesema anatarajia kukutana na mgombea wa chama tawala cha Jubilee Uhuru Kenyatta baadaye.

"Mkutano huo utafuatwa na mkutano wa pamoja wa wawili hao," ameandika kwenye Twitter.
Mkutano wa wagombea urais na IEBC Kenya waahirishwa
Gazeti la kibinafsi la Nation limesema wawili hao walikutana kwa takriban dakika 40 katika makao makuu ya tume hiyo Nairobi.
Mwenyekiti huyo alikuwa awali ameitisha mkutano wa wagombea urais wote leo adhuhuri lakini akauahirisha mapema leo asubuhi.

Hata hivyo, ingawa Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza yuko tayari kwa uchaguzi huo na utaendelea, mgombea wa upinzani Raila Odinga alijiondoa wiki iliyopita.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya awalaumu wanasiasa
Jana, Bw Odinga, ambaye ni mgombea wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) alitangaza kwamba siku hiyo badala ya kushiriki uchaguzi, wafuasi wake watafanya maandamano makubwa kote nchini.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati siku ya Jumatano alikuwa amewalaumu wanasiasa wa kusababisha kuwepo kwa mazingira yanayoifanya vigumu kuandaa uchaguzi huru na wa haki.
Alisema alikuwa anawapa "kadi ya manjano".
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang'i tayari ametangaza Alhamisi kuwa siku ya mapumziko.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad