Mkuu wa Wilaya Achoma Nyumba 900 Chunya

Mkuu wa wilaya ya Chunya, Bi. Rehema Madusa ameingoza Kamati ya Ulinzi na Usalama kuteketeza nyumba zaidi ya 900 za wananchi ambao wamevunja sheria kwa kuvamia na kuishi ndani ya hifadhi ya misitu ya asili iliyopo tarafa Kipembawe Chunya.

Kufuatia zoezi hilo la kuwaondoka watu hao waliovamia hifadhi hizo lililofanywa na Kamati ya Ulinzi kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu nchini, TFS, zaidi ya kaya 1000 zimekosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuchomwa moto.

Meneja wa wakala wa huduma za misitu (TFS) Grace Wille, wilaya ya Chunya amesema kuwa katika tarafa ya Kipembawe kuna misitu zaidi ya saba inayohifadhiwa, lakini misitu hiyo imevamiwa na makundi ya watu ambao wanaendesha shughuli za kiuchumi na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kwamba zoezi hilo la kuwaondoa ambalo limeanza leo litakuwa ni endelevu.
Mbali na hilo wananchi ambao wamechomewa moto nyumba zao wameonyesha kus
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. @Douglas Mmari, hao watu walishaambiwa kitambo, wakakumbushwa tena na tena wao wakaona la maana ni kuchangishana pesa kumpelekea Mbunge azuie zoezi. Ungefika eneo hilo na kuona walivyoharibu huo msitu ambao ni hifadhi hakika usingediriki kunena uliyonena, tusipoaangalia watu wa aina hii nchi hii itakuwa jangwa muda si mrefu.Usihalalishe waliyoyafanya hatua zilizochukuliwa ni stahiki period.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad