Sophia Mjema amesema hayo alipowatembelea wananchi hao ambao wamelalamika kufanyiwa fujo na kupigwa na askari hao kwa siku mbili kutokana na askari mmoja kuuwawa na watu wasiojulikana, Mkuu wa Wilaya anasema kuwa askari hao walipaswa kufanya uchunguzi kujua ni watu gani walihusika kufanya mauaji ya askari huyo na si kwenda kufanya fujo na kuwapiga wananchi pasipokuwa na sababu.
"Kama kuna askari alipatikana ameshafariki utaratibu ulikuwa uchunguzi ufanyike ili waweze kujiridhisha baada ya hapo wale ambao wangetambulika ndiyo wangechukuliwa hatua lakini kwa hili halikubaliki, kwa hiyo nasema hivi askari wote waliohusika kufanya fujo na vurugu wachukuliwe hatua za kinidhamu na huku barabarani sitaki kuona FFU yoyote anasumbua wananchi" alisema Mjema
Aidha Mkuu wa Wilaya huyo ametaka wananchi ambao wameumizwa na askari hao kwa vipigo kwa siku mbili mfululizo waweze kujiorodhesha kwa majina ili wapatiwe matibabu na kusema wale ambao wamepoteza mali zao utaratibu utafanyika kuona nini kifanyike.