Mo Dewji Aicheka Yanga Kwa Dharau Asema Hawataweza

Mo Dewji Aicheka Yanga Kwa Dharau Asema Hawataweza
Mfanyabiashara mkubwa nchini, Mohammed Dewji ambaye ni shabiki kindakindaki wa Simba amefunguka na kuwaambia wapinzani wao wa jadi Yanga kuwa hawataweza.

Mohammed Dewji ameweka picha ya katuni ambayo inamuonyesha mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba Ibrahim Ajib ambaye sasa anakipiga Yanga akifurahia ushindi wa bao kwa kuvua jezi yake namba 10 mgongoni baada ya kuitandika bao la pili klabu ya Kagera Sugar katika mchezo uliofanyika Jumamosi katika uwanja wa Kaitaba Kagera.
Kutokana na kitendo hicho cha Ajib kuvua jezi yake Mo Dewji anawasanifu wapinzani wake wa jadi Yanga kwa kuwaambia hawataweza kufunga goli zuri kama alilofunga Mshambuliaji wao wa kimataifa raia wa Uganda, Emmanuel Okwi na kusema kama ingetokea wangefunga goli kali kama hilo anaamini kuwa mchezaji wao huyo huenda angevua bukta kabisa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad