Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amekanusha tetesi za kufukuzwa uanachama na kujitapa kuwa yeye ni nyota ta ya chama.
Akizungumza jana kwenye mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi wa viongozi wa CCM Wilaya ya Geita, Msukuma alijitapa kuwa yeye ni nyota ya chama.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwenye mitandao ya kijamii zikimtaja Msukuma na wanachama wengine kuwa wamefukuzwa uanachama.
Katika hatua nyingine, Msukuma alisema uamuzi wa madiwani wa Wilaya ya Geita kudai fedha za halmashauri kwenye Mgodi wa GGM si wa kubahatisha, hivyo aliwataka madiwani ambao hawajaripoti polisi au kukamatwa waende ili wakahojiwe.
Msukuma ambaye pia ni Mbunge wa Geita Vijijini na madiwani, wanashtakiwa kwa makosa manne ambayo ni kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali, kufunga barabara na kusababisha wafanyakazi wa GGM wasiende kazini na kufanya uharibifu wa bomba la maji.
Alisema ni wajibu wao kuwekwa ndani kwa kuwa wanadai haki ya wananchi waliowaamini, hivyo hawana sababu ya kuogopa.
Mbunge huyo alisema licha ya kesi hiyo, tayari madiwani wengine wamefunguliwa kesi nyingine kutokana na kuwajadili watu waliotajwa kwenye taarifa ya mkuu wa mkoa iliyotolewa na kamati ya biashara dhidi ya wafanyabiashara wa Geita na Mgodi wa GGM.
“Kapaya na Bugomola wameshahojiwa kwenye kesi mpya na madiwani wote mliochangia siku ya kikao mmefunguliwa kesi nyingine eti mliwajadili watu, nashangaa kama madiwani wanazungumza kwenye vikao halali halafu wanakamatwa, basi bora tujiuzulu,” alisema Msukuma.
Matokeo ya uchaguzi
Katika uchaguzi huo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Muhoja Mapande alitetea nafasi yake kwa kupata kura 754.
Wengine na kura zao kwenye mabano ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, Constantin Morand (777), Herman Kapufi (681) na Leornad Bugomola (657). Nafasi za ujumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa ni Saashisha Mafuwe (913) na Rebeca Lusangija (663)
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Mapande aliwataka wanachama kutambua kuwa wajibu wa chama ni kuisimamia Serikali hivyo wakawasimamie watumishi wa umma kuanzia ngazi ya kijijini.
Msukuma Atamba Akanuisha Tetesi za Kiufukuzwa UIanachama CCM Asema Yeye ni Nyota ya Chama
0
October 09, 2017
Tags