Mtukufu Agha Khan Awaasili Nchini kwa Mwaliko wa Rais Magufuli

Mtukufu Agha Khan Awaasili Nchini kwa Mwaliko wa Rais
Kiongozi wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, Mtukufu Aga Khan amewasili nchini kwa mwaliko wa Rais John Magufuli.

Mtukufu Aga Khan amewasili leo Jumatano saa nne asubuhi na amepokewa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Dk Hussein Mwinyi na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Baada ya kushuka kwenye ndege, Mtukufu Aga Khan alikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Polisi na kutazama burudani ya vikundi vya ngoma.

Kiongozi huyo atakuwa na mazungumzo na Rais Magufuli baadaye mchana na kesho atahitimisha ziara nchini.

Mtukufu Aga Khan pia ni kiongozi mwasisi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan ambao unatoa huduma mbalimbali duniani.

Kwa Tanzania mtandao huo unatoa huduma za afya, bima, elimu, mikopo kwa wajasiriamali, kusaidia kilimo na hasa kwa wakulima wa vijijini.

Ziara ya Mtukufu Aga Khan inalenga kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na taasisi yake ambayo ina uwekezaji mkubwa nchini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad