Baada ya kukamatwa kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, Timu ya mawakili wa chama hicho kimeeleza kuwa kiongozi huyo amekamatwa na polisi na anahojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya uchochezi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Wa Sheria wa Chama hicho, Stephen Mwakibolwa, imesema kuwa juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, amekamatwa na polisi na kuhojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya Uchochezi juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo:
1. Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.
2. Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.
Zitto Kabwe amekamatwa leo asubuhi na kupelekwa katika kituo cha polisi Chango’mbe.
Mwakibolwa: Zitto Kabwe Ahojiwa Akituhumiwa Kufanya Makosa ya Uchochezi
0
October 31, 2017
Tags