Mwenge wa Uhuru Kuzimwa Visiwani Zanzibar Leo
0
October 14, 2017
Kutoka Visiwani Zanzibar, zinafanyika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo zinaambatana na maadhimisho ya miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hyati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Uwanja wa Amaan
Baada ya mwenge wa uhuru kuanzia mkoani Katavi, hatimaye leo Oktoba 14, umewasili na unatarajia kuzimwa katika uwanja wa Taifa wa Aman, kisiwani Zanzibar katika mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo mkuu wa mkoa huo, Ayoub Mohammed Mahmoud, ameukabidhi mwenge kwa serikali na umepokelewa na waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge, Kazi, Vijana, ajira na walemavu, Jenista Mhagama.
Baada ya makabidhiano hayo hafla hiyo itahamia katika kanisa la romani katoliki kwa ajili ya ibada maalum ya kumuombea na kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere, ibada hiyo itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, Makamu wake Samia Suluhu Hassan, Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na viongozi wengine waandamizi.
Tags