Nape Nnauye: Watu Hawatakiwi Kuiogopa Serikali Yao Bali Serikali Inapaswa Kuogopa Watu Wake

Nape Nnauye: Watu Hawatakiwi Kuiogopa Serikali Yao Bali Serikali Inapaswa Kuogopa Watu Wake
Mbunge wa Mtama, Nape Moses Nnauye amefunguka na kusema kuwa watu hawapaswi kuogopa serikali yao bali serikali ndiyo inapaswa kuogopa watu wake.

Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ametumia maneno ya mwandishi wa vitabu maarufu kutoka nchini Uingereza Alan Moore ambaye mpaka sasa ameshaandika vitabu vingi vikiwepo Watchmen, V for Vendetta na From Hell.
Ujumbe huo alioweka Mbunge wa Mtama uliwekwa kwa lugha ya kiingereza " “People shouldn't be afraid of their government. Governments should be afraid of their people”  ukiwa na maana ya kuwa Watu hawapaswi kuogopa serikali yao bali Serikali inapaswa kuogopa watu wake.

Kufuatia ujumbe huo baadhi ya watu wameungana naye na kusema ndiyo ambavyo inapaswa kuwa huku wengine wakimpa changamoto kiongozi huyo


Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kaka Nape sijasoma habari nzima ila ningeongeza, raia mwema asiogope labda waasi ndo waogope

    ReplyDelete
  2. You are 100% correct. Nakuunga mkono asilimia 100. Inabidi uongeze haya. Watu ndio hufanya serikali. Bila watu hakuna serikali. Na viongozi wote wa serikali huchaguliwa na watu. Ukimchagua raisi, unampa madaraka ya kuteua viongozi wachache kama watumishi wa serikali. Inamaana watumishi wa watu.
    Kama Watanzania wote wanalijua hili, wengi wanaoshangilia maovu viongozi watendapo kazi wasingefanya hivyo. Sisi watu tunataka maendeleo. Tunatunga sheria ili zitusaidie, zitulinde, na kutuongoza. Hakuna mtu juu ya sheria. Ikiwa wote tunaamini hivi, Hakuna Mtanzania hata mmoja atakayekubali kuendeshwa na akili mmoja bila kuthamini akili ya wengi. Na kila Mtanzania angedai Katiba na kuiheshimu katiba. Tungelilia katiba safi ili wote tuitii na kuifuata. Na kusingekuwa na kiongozi yeyote anayeamuru mtu yeyote atiwe ndani bila kufuata chombo cha sheria. Hana mamlaka. Na wengi wangejifunza kutii sheria wakijua watachukuliwa hatua kali zinazoendana na makosa bila upendeleo wowote.
    Kuna upendeleo bado nchini. Kwa viongozi kupitia chama, wadhima, na undugu na ukabila bado upo ingawa uliondolewa na ndugu Nyerere, wengi viongozi wanalitumia nina lake visivyo. Na inasikitisha Watu wawaogope viongozi wao ambao wamewachagua. Mtu umempa kazi na inabidi akusikilize, akuelewe, akujali, akuheshimu, na akufanyie kazi uliyompa kama unavyotegemea afanye. Asipofuata matakwa hata yeye aadhibiwe na sheria itumike sawa na mwananchi. Hii elimu kila mtu akiijua watu hawatamwogopa kiongozi yeyote sababu kaajiliwa tu. na watakuwa huru kumkosoa, au kumshauri waonapo anakwenda kinyume. Lakini kwa miaka yote tunatawaliwa kiknguvu. Watu bado hawazijui nguvu zao. Na wengi wanavyoamka nchi itabadirika tu. Watu watajisikia huru kutoa mawazo , kujieleza, na kudai haki zao sababu wamewaajili watumishi wa serikali na wanawalipa kila mwezi. Iwe kama mwajili wa biashara. Kama mwajiliwa hafai unaweza mfukuza kama haonyeki. Maongezi kama haya ndiyo yanayotupanua mawazo. Nafurahi kuwaona wabunge na mawaziri wachache toka CCM kuamka na kujisikia huru kuchanganua mambo badala ya kusalimu amri kwa mkuu au toka juu na kusahau kwamba kazi zao ni kuwawakilisha wananchi jinsi watakavyo na si kwa kuwaamrisha. Ni kinyume kabisa cha uongozi.Elimu safi kwa Taifa zima kuanzia majumbani, shuleni na makazini lazime vianze upya kwa jambo hili. Tumeuua undugu. Umoja. Tumeua Amani ambayo kwa miaka mingi imetulinda.

    ReplyDelete
  3. I am totally happy with the government. Nothing wrong with it. Please do not get discouraged Mr magufuli we are supporting you. It is difficult to please every person's interest. The important thing is you are working for the interest of the vast majority. God bless you.

    ReplyDelete
  4. Its impossible to find any government with no problem. No such a thing. We like our president no doubt. But we would like to see the freedom of speech. Not to shut down news papers, or stop people from speaking out. This is what makes the country better. When you allow people to exchange ideas, it open up peoples horizons. once you stop it, people become fearful, and lazy thinkers. I don’t know where you reside. Many countries which allow freedom of speech becomes more successful.I cant imagine if indeed you support the killing of the people too buy wasiojulikana. It cant go on like this e and allow people to fear the ruling power. That must not be tolerated. These are our fellow Tanzanians for God sake.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad