Nassari, Lema Waanika Ushahidi wa Rushwa Dhidi ya Madiwani Waliohamia CCM

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari ameweka hadharani ushahidi wa rushwa na waliopewa madiwani ambao wamejiuzulu Chadema kwa madai ya kumuunga mkono Rais Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Nassari ambaye ameambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa ushahidi huo na kueleza wataukabidhi Takukuru na katika taasisi nyingine.

Katika ushahidi wa video  uliorekodiwa viongozi kadhaa wakiwema Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa (H) Meru Christopher Kazeri wamesikika wakiwashawishi madiwani kuhama na baadhi waliahidiwa wangelipwa posho za vikao vyao vilivyobaki hadi 2020 na kukamilishwa miradi yao.

Miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa wapewe fedha na kupata ajira na kukamilishwa miradi yote ya maendeleo waliyoahidi ikiwa ni pamoja na wengine kubadilishiwa makazi pamoja na diwani mmoja kusaidiwa gharama za kufanikisha harusi.

Hata hivyo Mbunge Nassari pamoja na Godbless Lema wameahidi kesho watadfika katika ofisi za TAKUKURU Dar es salaam kwa ajili ya kuukabidhi ushahidi huo wa rushwa kwa Mkurugenzi  Valentino Mlowola

Pamoja na hayo wakati Nassari akiutoa ushahidi huo hadharani leo tayari madiwani 10 wa Chama chake wameshapokelewa ndani ya CCM huku wengie wakiwa wamepinga vikali kuhama chama hicho kwa sababu ya rushwa.

Aidha Nassari amesema ameamua kutoa ushahidi huo sasa kwa sababu alikuwa akiendelea kukusanya ushahidi wa kutosha.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad