Nilitegemea Hili Kutokea- Zitto Kabwe

Baada ya Kampuni ya uchimbaji madini nchini, Accacia kudai kwamba haina pesa za kuilipa serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa jana na kampuni ya Barrick Gold Mining,  Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwamba Serikali ilikosea kutangaza ushindi mapema.

Mh. Kabwe amesema alitegemea kauli kama hiyo kutoka kwenye Kampuni ya Accacia kwani siyo mara ya kwanza kwa Kampuuni ya Barrick kutoa ahadi kama hiyo (ameiita kishika uchumba) kwani hata 2016 walipobanwa na bunge kuhusu suala la misamaha ya kodi.

Mh. Zitto amesema kwamba tangu jana alishangaa sana kusikia serikali ikisema kwamba "Tumefanikiwa" kwani haikuwa ikizungumza na kampuni ya Accacia bali mmiliki wa kampuni Barrick na kutokana na sheria ya Makampuni Mmiliki kama mmiliki anasimama mwenyewe na kampuni husimama yenyewe.

"Nilitegemea hili kutokea baada ya serikali kutangaza hayo jana. Ni makosa tuliyoyafanya wenyewe. Serikali kutangaza ushindi kwenye mazungumzo waliyofanya na kampuni hiyo yalikuwa ni makosa kwani ni kawaida kwa kampuni ya Barrick kutoa ahadi kama waliyokuwa wameitoa jana na walishafanya hivyo kwa nchi ya Bolivia, na Chille. Serikali inapaswa sasa irudi kukaa mezani na Accacia wenyewe kwa ajili ya mazungumzo".

Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa haina uwezo wa kulipa dola milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa mtanzania yeyote anaefuatilia hali ya siasa na wanasiasa nchini anajua kabisa matokeo yoyote mazuri yatakayotokana na mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea baiana ya serikali na Acacia yangelimkera Zito kabwe tena sana yaani huo ndio ukweli wenyewe. Zito kabwe anasema ameshamgaa kusikia serikali kutangaza ushindi? Siob tu kwmaba Zito alishangaa na taarifa za ushindi kwenye madai yetu isipokuwa taarifa hizo za ushindi kwa nchi ya kufunga mikataba mipya ya maana na kampumi hiyo ya madini hakika zilimsikitisha na kumsononesha sana Zito Kabwe. Zito Kabwe anafurahia mabaya kwa nchi yetu. Kama Zito anaishangaa serikali kutangaza ushindi sisi watanzania tuliowengi tunayoiyoombea mazuri nchi yetu tunamshangaa sana Zito kabwe kukimbilia kuzungumzia suala ambalo kiuhalisia hana uweledi nalo. Zito amepata ahueni na furaha baada ya kusikia taarifa yakuwa kampuni hiyo haina pesa ya kuilipa Tanzania. Yaani papara za zito katika suala hili ni sawa na mtu aliekimbilia usafiri wa basi au daladala na kupanda bila ya kuangalia linapokwenda. Zito hata akijaribu kufanya nini ili awasibitishie watu kwamba yeye yupo sahihi katika suala hili ni kupoteza muda wake na kuharibu zaidi. Watanzania wameshamuelewa ni mtu wa aina gani. Yeye Zito kabwe kaona million mia tatu ni suala pekee lilokuwa likijadiliwa katika mazungumzo yale? Kilichokuwa kinajadiliwa pale hasa ni mikataba ya maana kwa nchi yetu na kwa furaha kubwa serikaliimefanikiwa kwa hilo. Lakini Zito Kabwe hawezi kulizungumzia hilo la mikataba kwa sababu hakufurahia kwa nchi yetu kufanikiwa kufunga mikataba
    Ya maana. Msimamo wa Maghufuli upo pale pale na watanzania tunaimani kwa kila ambacho serikali inakidai kutoka Acacia basi hapana shaka yeyote kitapatikana it is about time kwani kama ni ugonvi wa kugombania kisu basi sisi ndio tulioshika mpini hao Acasia wao wenyewe taabani baada ya kuzuiwa kwa makinikia.

    ReplyDelete
  2. Zito mbona kiherehere?
    Wewe ni mtu mzima sheikh, ebo!
    Issue ya Serikali ina heshma zake.
    Unataka kutuonesha nini?
    Si kila issue iwe ya kusiasa.
    Kwani kimbelembele cha nn?
    Kaa pembeni acha vidume vyetu vifanye kazi.
    Issue yako ya kupoteza viongozi ndio hot cake yako kwa sasa. Serikali imefanya kazi kubwa kufanya muafaka na Barrick, and that was the most significant step. Na ule ndio ushindi kwa Taifa. Kusema hawana hixo pesa wewe kaa chonjo acha Serikali idili nao.
    Jifunze kukaa kimya kijana, hii si issue ya bungeni. Tais toi!!

    ReplyDelete
  3. Huyu jamaa sijui ana matatizo gani. Can you imagine uishi na mtu mwenye kiherehere cha kiwango hichi au ufanye nae kazi sehemu mmoja!! Nadhani ndio maana Mbowe yalimshinda aisee.

    ReplyDelete
  4. Nyie wote mliotoa mawazo hapo juu hamjielewi .zitto kasimama kwenye ukweli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukweli kuhusu nini? Mara ya kwanza alisema hizo pesa ni kidogo, mara hii anasema 'nilijua hawatalipa' TUMUELEWEJE?? Hebu 'chapeni lapa', mtuwache na Tanzania na Magufuli wetu .........hovyooooo

      Delete
  5. Mhhhj...Zitto hajielewi Na anatafuta Ajira nasikia Ile ya kigamboni itabidi arudishe kwa serikali maanake ulikuwa Ni mgao..kwa hiyo Ni lazima apigeke kelele Ili ifunike...TUMEKUSTUKIA NA TUNAKUJA HUKO...
    JITAYARISHE

    ReplyDelete
  6. Utegemee
    Usitegemee..!!
    Wewe Ni nani????
    Khabithi al amali.
    YANAKUSHINDA NA YATAENDEKEA KUKUSHINDA.
    MWACHENI MH RAISI AENDELEE JUTUBADILISHIA NCHI YETU.

    WEWE UNATIAKITI JOTO BUNGENI SASA NI MIAKA MINGAPI?..??!!!!!
    JE UKIJOTATHMINI UMEWAPELEKEA MAENDELEO GANI WALIOKUPA DHAMANA. .???
    NI ULAHI NA FESI BUKU NA TWITA
    WACHA POLOJO POLOJO HUU SI QAKARU WAKE.
    AWAMU HAINA UPUYZI WA KUKUBEBA KAMA ULIVYOZOEA HUKO NYUMA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad