Nipo Tayari Kuwajibika Endapo Rais Ataruhusu- Zitto Kabwe

Nipo Tayari Kuwajibika Endapo Rais Ataruhusu- Zitto Kabwe
Mbunge na kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa yupo tayari kuwajibika kuhusu kinachodaiwa kupika taarifa za serikali endapo Rais Magufuli ataruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye mapato ya mwezi Julai na Agosti 2017.

Zitto Kabwe amesema kuwa wao wanatumia takwimu za serikali kuwaonyesha wananchi kuwa serikali yao inadanganya na haisemi ukweli wote na uhalisia wa uchumi na kuporomoka kwa mapato. Zitto Kabwe amedai kuwa kodi inayokusanywa na TRA nchini inaweza kulipa mishahara na kuhudumia Deni la Taifa tu na si vinginevyo.
"Kwanini Rais wetu hasemi kuwa tunakopa? Kukopa sio dhambi, kwanini aaminishe watu kuwa anatekeleza miradi kwa kuwa kodi zimeongezeka? Kama Rais anaamini kuwa mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye mapato ya Julai na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi kwa umma. Rais akifanya hivyo nitawajibika" alisema Zitto Kabwe.

Jana Rais John Pombe Magufuli alisema kuwa kuna watu wanapika taarifa za serikali na kusema uongo na kuvitaka vyombo vya usalama na  Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kuwashughulikia watu hao ikiwezekana wafungwe kabisaa

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. zitto acha upuuzi wewe acha kutokwa na povuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  2. chama chako kimekushinda tupe takwimu za chama chako kwanza kwa nini unakimbiwa

    ReplyDelete
  3. Ajakimbiwa wale wamerudi home .zitto endelea kutuambia ukweli baba .werevu tumeshaelewa

    ReplyDelete
  4. ivi unaweza kunipa takwimu za migebuka

    ReplyDelete
  5. wamerudi baada ya kuona kule wengi ni wazee wa ten pasenti pia werevu tumeshaelewa HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  6. ZITO KULA KIMYA KIMYA TUNAJUA UNATUMIKA

    ReplyDelete
  7. Sema usioogopee seema.cc vijana tunahitaji mageuzi seema!!!

    ReplyDelete
  8. We dogo zitto, usitafute ligi na JPM si'saizi yako, pambana na 'wamchangani' wenzako mfyuuuuuuuuuuuu akope, aibe, hayakuhusu, cha muhimu ni KAZI-TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad