Msigwa amesema kitendo cha Nyalandu jana kuamua kuachana na Chama Cha Mapinduzi ni wazi kuwa amethibitisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) si chama tena bali kimekuwa chini ya dola na hakina uwezo wa kuikosoa serikali tena. Msigwa aliainisha mambo hayo saba kama ifuatavyo
1. Nyalandu umethibitisha kwamba CCM sio Chama Cha siasa tena. CCM iko chini ya miguu ya dola na haina uwezo wa kuikosoa serikali tena
2. CCM imepoteza mwelekeo wake. Imeshindwa kusimamia uchumi, siasa na uongozi wa nchi
3. Misingi ya nchi yetu imebomolewa chini ya utawala wa CCM na umeitisha mwito wa kila mmoja wetu kuijenga upya misingi ya nchi yetu
4. Tanzania imekithiri ukiukwaji wa haki za binadamu , dhulma na kutekwa na serikali mhimili wa bunge pamoja mahakama.
5. Watanzania wapate fursa ya kuchagua itikadi wanayoona inafaa na sio kutishiwa na kulazimishwa.
6. Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini yatapatikana kwa mfumo wa demokrasia na Uhuru wa mawazo.
7. Mwisho umeonesha umuhimu wa kupata Katiba Mpya kwa sasa katika Nchi yetu
Mbali na hilo Mbunge Msigwa alimaliza na kusema kuwa "Kuishi nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inawezekana"
Hamna lolote wapiga dili tu nyie, hivi si wewe uliesema anayemuunga mkono Lowassa apimwe akili haraka, sasa nani hapo ataaendelea kuwaamini ninyi. Jamaa kaepa aibu ya kuondolewa hana jipya.
ReplyDeleteIdiot paster, what Kind of mchungaji huyu mtu, kutwa kupayuka payuka ujinga, hata kama mazuri wao hawayataki, au ndio kutaka kukimbilia uongozi, Hamna dili Sasa hivi, upepo umebadili njia ya kuvuma, hapa wote sawa Sasa, Masikini au tajiri wote sawaaa, ndio huko anakotupeka mmjomba Magu Yaani khali ya usawa, kama ni cake ya Taifa angalau tupate kwa usawa,
ReplyDelete