Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilikurupuka kuchukua uamuzi wa kuunga mkono Chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Polepole amesema Chadema walikosea kushabikia uchaguzi wa Kenya kwa kuonesha upande fulani kati ya vyama vinavyoshindana kuomba dhamana kwa wananchi wake kuongoza nchi hiyo na kudai kitendo hicho sio cha kikomavu kwenye siasa.
“…Walikurupuka kuchukua upande kwa sababu katika diplomasia na mashirikiano ya nchi huwa ni dhambi kubwa kwa nchi moja au chama cha kuanza kuingilia uchaguzi wa nchi nyingine na kuchukua upande katika pande zile zinazoomba dhamana kwa wananchi katika nchi nyingine ambayo siyo ya kwenu.“amesema Polepole kwenye mahojiano yake na Times FM huku akielezea madhara ya kitendo hicho.
“Fikiria mfano unachukua upande kwenye uchaguzi wa Kenya halafu wewe ni chama kilichopo madarakani hapa Tanzania halafu upande kule wanashinda wengine sio wale uliowaunga mkono. Tafsiri yake nini nini? umeharibu mahusiano ya diplomasia utakuwa umejenga uadui..kwa sababu katika siasa watu wanatafuta dhamana kwa wananchi. Sasa hapa (Tanzania) kama kuna chama cha upinzani kilicho makini kinatakiwa kifahamu diplomasia na uhusiano ya kimataifa unatutaka sisi kuheshimu matakwa ya wananchi wa Kenya wao waamue watakayeona anafaa kuiongoza Wakenya, Kisha sisi tutalazimika kushirikiana na yeyote atakayepewa dhamana ya kuiongoza nchi hiyo.”amesema Polepole.
Hata hivyo, Humphrey Polepole amedai kuwa Chama chake cha Mapinduzi hakiwezi kuonesha kipo upande gani kwenye uchaguzi huo kwani kinajua fika kuwa dhamana ya kuongoza nchi hiyo ipo mikononi mwa Wakenya.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilitangaza mapema mwaka huu kabla ya Uchaguzi nchini Kenya kuwa kinamuunga mkono Rais Kenyatta katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu nchini Kenya.
CHADEMA NI 'UTOTO' TU, WAKIKUA-WATAACHA
ReplyDeleteCCM NI UZEE TU WAKIFA TUTAPUMZIKA
DeleteChadema ni vilaza wakiongozwa na kilaza mkuu Lowasa. Vichwa tope tupu hao yaani Chadema kuwa chama kikuu cha upizani kwa staili yao ni faraja kwa CCM wanajua hawana mpizani wa kweli badala ya mitusi na ubishi wa kipumbavu. Tanzania hakuna chama kukuu cha upizani kwa CCM Kwani upizani sio mitaani bali upizani ni Bungeni. Chama gani chenye idadi ya wabunge sawa au karibu na ya wabunge wa CCM Bungeni wanaoweza kuwazuia CCM kupitisha miswaada inayoletwa bungeni?
ReplyDeleteDr Slaa kaondoka na chadema yake
ReplyDelete