Rais Magufuli Afunguka Kuhusu Bombardier

Rais Magufuli Afunguka Kuhusu Bombardier
Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kuzungumzia juu ya ndege za Tanzania sita zilizonunuliwa na serikali ikiwepo Bombardier Q 400-Dash ambayo inashikiliwa nchini Canada na kusema ndege hizo zitawasili nchini mwakani 2018.

Rais Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, Rais Magufuli amesisitiza kuwa Tanzania inakosa watalii wengi kutokana na kukosa ndege.

"Tumenunua ndege sita ndege mbili zimeshawasili Tanzania, lakini ndege zingine ikiwepo Bombardier zitawasilia mwakani 2018 mwanzoni tunafanya haya kwa ajili ya kutengeneza Tanzania mpya, nchi ambazo zina ndege zake idadi ya watalii wanaoingia kwenye nchi hiyo ni kubwa zaidi, nchi yetu ni ya pili kwa kuwa na vivutio vingi duniani lakini idadi ya watalii wanaoingia ni ndogo kutokana na kukosa ndege zetu" alisema Rais Magufuli 

Serikali ilikiri ndege mpya aina ya Bombardier Q-400 Dash 8 iliyonunuliwa na serikali ambayo ilipaswa kuingia nchini toka mwezi Julai lakini ikashindikana kufika kutokana na kudaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd iliyozuia ndege aina ya bombardier Q400-Dash 8 iliyonunuliwa na Tanzania nchini Canada.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ndo kasema nn. amekuwa kama Le madolezzz. Kibamia akili moja.

    ReplyDelete
    Replies
    1. punguwani huna akiri kabisa, kwani wewe huoni kilichoandikwa? au akiri yako iko matakoni mjinga wewe? rudi shule kafundishwe kinachoandika na uombe uelewa kutoka kwa Mungu chizi wewe

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad