Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amewagiza watendaji wa Wizara ya Elimu kuhakikisha wanatoa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wenye sifa ya kupata mikopo kabla ya vyuo kufunguliwa ili kuepuka kupata usumbufu wakati wa masomo yao.
Rais Magufuli ameyazungumza hayo baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua Ikulu jijini Dar es Salaam,amesema tarehe 29 mwezi uliopita.
“Tarehe 29 mwezi uliopita wizara ya fedha imetoa Shilingi bilioni 147, zimepelekwa Wizara ya Elimu, ni mikopo ya wanafunzi wenye sifa, nitashangaa kama watakuwepo wanafunzi ambao hawatapata mkopo, nitashangaa” amesema Magufuli.
Rais Magufuli amewaapisha Makatibu Wakuu wapya, Naibu Makatibu Wakuu wapya na Wakuu wa Mikoa wapya baada ya kuwateua juzi, waliapisha jana Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Magufuli Amewaagiza Watendaji wa Wizara ya Elimu Kuhakikisha Wanatoa Mikopo kwa Wanafunzi
0
October 28, 2017
Tags