Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema yuko tayari kubadilisha sheria ili kuweza kuwalinda wanachi wanaotakiwa kupitiwa na bomoa bomoa mkoani Mwanza, kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege na miundo mbinu mingine.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akihutubia taifa kwenye sherehe za uzinduzi wa daraja la Furahisha la mkoani Mwanza, na kusema kwamba serikali yake haiko tayari kuona watu wakionewa , hivyo yuko tayari kuwalinda hata kwa kubadilisha sheria itakayowaruhusu wananchi hao waendelee kuishi hapo.
"Tuliwatazama watu wakajenga wakaweka 'Investment' zao, sasa leo tunawafukuza, tusubiri kwanza, inawezekana walifanya makosa lakini kwa sababu serikali yangu ina huruma nasema ndugu zangu msiwabomoleshe, yapo maeneo ambayo kwa kweli itabidi watu wahame, mfano wale wa uwanja wa ndege, kama kuna mahali pa kubadilisha sheria mimi nitazibadilisha ili kusudi baadhi ya wananchi waliojenga pale miaka 30 tuweze kuwalinda na kukaa pale na kuendesha maisha yao", amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli leo yupo mkoani Mwanza kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili, ambapo pia licha ya uzinduzi wa daraja la Furahisha, anatarajiwa pia kuzindua kiwanda kimoja.
Rais Magufuli Asema Yupo Tayari Kubadirisha Sheria Kuwalinda Wanaotakiwa Kupitiwa na Bomoabomoa
1
October 30, 2017
Tags
Muamba ngoma huvutia kwake
ReplyDelete