RAIS John Magufuli ambaye leo Oktoba 14, 2017 ni Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge amesema amejisikia faraja kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki maadhimisho hayo tangu awe Rais.
Aidha, Magufuli amemuelezea Hayati Mwl. Nyerere kama kiongozi shupavu alipeginani maslahi ya wanyonge na kupambana na wakoloni katyika kufanikisha kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika, Zanzibar na nchi nyingine za Afrika.
Amesema Nyerere alianza harakati za siasa mwaka 1953 baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha TAA ambacho baadaye kilizaa TANU huku akiwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari ambayo kwa sasa inaitwa Pugu Sekondari ambapo baadaye aliacha kazi hiyo ya kiufundisha na kujikita kwenye siasa za ukombozi.
Magufuli piua amesema iwapo Mwl. Nyerere angekuwa kiongozi mwenye tamaa au mbinafs, basi angechukua fukwe zote za Msasani, jijini Dar es Salaam na kuzifanya ziwe za mali yake, lakini hakufanya hivyo kwa sababu ya uzalendo mkiubwa aliokuwa nao.
Rais amesisitiza kuwa kamwe hatokukubali mbio za Mwenge wa Uhuru zifutwe katika kipindi chake cha uongozi, kwani mwenge huo una manufaa makubwa kwa Taifa ikiwemo kuzindua miradi mbalimbali za maendelo pamoja na kuwa nembo muhimu kwa Taifa letu.
Amesema wanaotaka mwenge huo ufutwe huenda hawajui historia ya nchi hii na kwamba kama wanaweza kukubali fimbo na kombe la dunia vikaletwa nchini na wakavipokea basi mbio za mwenge ni muhimu zaidi kuliko wanavyodhani.
Akizungumzia hali ya uchumi wa nchi, rais amekanusha wanaodai kuwa uchumi umeshuka huku akieleza kuwa uchumi wa Tanzania unazidi kupanda hukui mfumuko wa bei ukishuka na matokeo yake yanaonekana kwenye bidhaa pamoja na kushuka bei zake. Pia ameeleza kuongezeka kwa viwanda na wawekezaji wa kibiashara hapa nchini.
Rais Magufuli: Kamwe Sitokubali Mbio za Mwenge Zifutwe Katika Uongozi Wangu
0
October 14, 2017
Tags