Rais Mugabe Avuliwa Wadhifa..Kisa Wakosoaji

Shirika la afya duniani WHO limefuta uteuzi wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, kama balozi wa nia njema wa WHO.


"Nimesikiliza vizuri wale wote ambao wameelezea hisia zao," mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema katika taarifa.


Awali alikuwa ameisifu Zimbabwe kwa kujitolea kuboresha afya ya umma.


Lakini wakosoaji walisema kuwa mifumo ya afya nchini Zimbabwe iliporomoka nchini ya utawala wa Mugabe wa miaka 30.


Wafanyakazi mara nyingi hukosa kulipwa na madawa wakati mwingine hukosekana huku Mugabe mwenyewe mwenye umri miaka 93 akiwa anasafiri nje ya nchi kupata matibabu.


Bw. Tedros alisema ameongea na serikali ya Zimbabwe na kuamua kuwa kumvua Mugabe wadhifa huo ni kwa manufaa ya WHO.


Alisema anasalia kujitolea kufanya kazi na chi zote na viongozi wake kujenga huduma bora za afya.

Uteuzi wa Bw. Mugabe ulipatawa na shutuma kali, Serikali ya Uingereza, waziri mkuu wa Canada na mashirika mengine kadha pamoja na watumiaji wa mitandao ya kijamii ni kati ya wale ambao walikosoa uamuzi huo.


Kufuatia kukosolewa kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu na kushangazwa kwa mataifa mengi wanachama, WHO haikuwa na lingine ila kufuata mpango wake wa kumvua Robert Mugabe wadhifa wa balozi wa nia njema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad