Serikali imesema Ufugaji Kuku, Samaki ni Uchumi wa Viwanda

Naibu Waziri wa Mifugo na Kilimo, Abdallah Ulega akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mwandege wakati wa kuhitimisha ziara yake iliyokuwa ya siku mbili.

Ulega aliyasema nayo wakati wa ziara yake  aliyoifanya Wilaya ya Mkuranga-Pwani kwenye vijiji Vinne ,ambapo  alisema hakuna sababu ya wananchi wa Mkuranga kuchukua Kuku mikoa mingine  wakati wanaweza kufuga wenyewe na kujipatia kipato na maendeleo yakapatikana na kuwawezesha kuuza hata sehem nyingine.
Amesema yuko tayari kuwasaidia wananchi wa Mkuranga mbegu za Kuku pamoja na watalaam wa kuwafundisha jinsi ya kufanya ufugaji wa Kuku na samaki wa kisasa.

Amesema ajira katika Wilaya hiyo zipo ikiwa ni pamoja na ufugaji Kuku pamoja na samaki ambayo ni ajira ya kudumu na soko ni kubwa kutokana mahitaji ya vitoweo hivyo kuhitajika kwa wingi.

"Sioni sababu wananchi wa Mkuranga kuchukua kuku kutoka mikoa mingine wakati mnaweza kufanya nyinyi wenyewe kutokana na maeneo mlionayo, haitawezekana kama nyinyi hamtaweza  kuonyesha mfano nikiwa ni Mbunge na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi"alisema Ulega.

Katika ziara yake  alitembelea Ujenzi wa Zahanati za Kibamba, Kimazichana na Mwandege na kuahidi kuwaunga mkono wananchi katika juhudi mbalimbali wanazoonyesha katika maendeleo ya huduma za jamii.

Ulega amesema kuwa wakati uliopo ni kufanya kazi za Maendeleo kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli juu ya dhamira ya serikali ya Viwanda.

 Naibu waziri  aliaahidi kuchagiaji  sh. Milioni moja na mifuko ya saruji kwa ajili ya kikundi cha VICCOBA cha wanawake waliojenga ukumbi wa mikutano na sherehe kilichopo Mwandege.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad