Serikali yakanusha Kukataa Kuongeza Mishahara, Yadai Taarifa hiyo ilizushwa na Chadema

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli hakuna sehemu ambayo alitamka kutotekeleza ongezeko la mwaka la mishahara ya watumishi wa Umma na kuitaka TUCTA kuachana na masuala ya siasa.

Hayo yamesemwa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas  kuwa hoja ya Rais Magufuli kutokuwaongezea mishahara watumishi wa Umma ilizushwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusema Rais Magufuli hakusema jambo hilo .



“Hakuna mahali Rais Magufuli alipokataa kutekeleza ahadi ya ongezeko la mwaka la mishahara ya watumishi wa umma, Serikali imetenga Bil. 487.7 kuwalipa wafanyakazi wanaopanda madaraja kwa mwaka huu wa fedha”amesema Dkt. Abbasi .

Soma taarifa kutoka serikalini kwa vyombo vya habari.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad