Serikali Yatoa Yafunguka Kuhusu Barrick

Serikali Yatoa Yafunguka  Kuhusu Barrick
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Katiba Na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi imetoa ufafanuzi kuhusu suala la faida na mgao wa asilimia 50/50 na kusema jambo hilo limekuwa halifahamiki vizuri kwa watu wengi.

Profesa Kabudi amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itapata asilimia 16 ambazo zinapatikana bila malipo kwa mujibu wa sheria za madini kama ambavyo zimepitishwa huku Barrick wao wakibaki na asilimi 84.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hebu msituchanganye na nyinyi, huyo profesa Kabudi alitoa hotuba nyingine tofauti na ile tuloisikia wote?

    ReplyDelete
  2. Kwa hiyo 16% ni 50%? Huo ni ufafanuzi gani ambao haujafafanua chochote!

    ReplyDelete
  3. Hiyo bado ni ya kizamani. Tanzania inahitaji 50% ya mikataba yote kwa sasa . Si 16. Mtanzania hatafaidika kamwe kwa namna hii.mnakumbuka ccm mlipopeleka swala hili kama dharura, na wapinzani waliwaulza kwa nini harakaharaka. Botswana mmeshindwa kuiiga ni nchi ya kiafrika ambapo Tanzania mliambiwa wazi igeni Botswana na muombe msaada huko. Mmewaponda washauri hao, mkawaleta wazungu wenye kupigania maslahi binafdi. Swali, hivi tukigundua mnatuengua na tukajulishwa kati ya viongozi wahusikao kusain mikataba hii wanakitu pia kule ndani. Kwa nini kati ya ushauri wote mliopewa mnakubali kiasilimia kifogo tu. Mkijua wazi wsmedhafaidika sana miaka yote hii. Na kwa nini bado waendelee kuwa mabwana wa mali za afrika hasa Tanzania mkijua wazi mnaweza kulipatia Taifa asilimia 50. Si kwa vile mlikuwa wachache, mliwaacha nje wapinzani wote ambao wangejitosa hasa asilimia mia moja kipata nusu, nusu. Mkiwa bado mnataka kuwaaminisha watanzania kuwa Raisi anajitosa, lakini vilevile bado hamjashirikiana na vyama vyote kama mlivyoshauriwa kuinusuru nchi. Na hii ni aibu kubwa kwa wadomi wetu kutokujali umoja , ushitikiana katika kulivuta gurudumu la nchi yetu jinsi inavyostahili kwenda. Bafo mnarudisha taifa nyuma. Na hiki ndicho chanzo kikuu cha kutokuelewana kwa mambo mengi kati ya uongozi wa CCCM na upinzani. Wenye akili wanafuatilia kila hatua na kuona uswahili inaotumika kiuongozi na kujisifia kwa viongozi wa juu hadharani mbele ya wazungu hao kwa kujipatia 16% tu kati ya mia. Na hii bado haiko wazi kama ni kwa madini safi au makinikia tu. Wamedhanufaika tosha. Bado wanawadanganya hawapati faida. Halafu ni wao tu watakao danganya tena kuwa wanapata hasara. Nani anafanya biashara kwa hasara miaka yote hii. Walikubali kuja kupigania maslahi ambayo si yao. Hii ni temporary ambayo mmeikubali lakini naliomba bunge lirudie masuala yote ya mikataba. 50/ 50/.Kwa madini yote hasa kwa hawa ambao wamedhafaidika toka. Uchumi na hawa wauchumi na washauri are not fit kufanya haya.tuwatafute wenye ujasiri zaidi ya kukaa na kuwaface mabepari bila woga na wanaojiamini hasa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad