Sheik Ponda Aelea Alivyoguswa na Hisia za Tundu Lissu Wakati Walipokuwa Wanabadirishana Mawazo

Sheik Ponda Aelea Alivyoguswa na Hisia za Tundu Lissu Wakati Walipokuwa Wanabadirishana Mawazo
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda amesema ameguswa na hisia za Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

Ponda amesema hayo leo Jumatano akizungumzia safari yake ya Nairobi nchini Kenya alikokwenda kumjulia hali Lissu hivi karibuni.

“Tulipokuwa tunabadilisha mawazo, niliguswa na hisia kubwa, badala ya mimi kumpa matumaini yeye ndiye alinipa matumaini,” amesema Ponda.

Amesema madhumuni ya safari yake yalikuwa kumjulia hali Lissu, kumwombea dua, kumjengea matumaini ya afya na kujenga mazingira mapana yanayotosha kulizungumza jambo lililomfika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad