Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Kutoa Msimamo wao Kauli ya Rais Magufuli

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limesema linatarajia kutoa msimamo wao hivi karibuni kufuatia kauli ya Rais Magufuli ya kutoongeza mshahara, mara baada ya vikao vyao na serikali kufanyika.

 Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Katibu Mkuu wa TUCTA, Yahya Msigwa amesema wanakusudia kuonana na uongozi wa serikali ili kujadili suala hilo, na ndipo watatoa msimamo wao kama hawatafikia makubaliano mazuri.

“Tunahitaji kuonana na uongozi wa serikali tujadili, kuna mambo mengi ya kujadili sio la mishahara tu, kwa muda mrefu vikao vimekuwa havikaliwi, hata vikikaliwa havina majibu, sasa hivi lazima tulitafutie ufumbuzi kwa sababu changamoto ni nyingi, wafanyakazi hawana hali nzuri kabisa, malalamiko ni mengi mno”, amesema Yahya Msigwa.

Hapo jana Rais Magufuli ametoa kauli ambayo imeibua sintofahamu nyingi kwa wananchi, baada ya kusema hajaongeza mishahara na hatoongoze mishahara kwa wafanyakazi kwa kipindi chote atakachokuwepo madarakani.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Enter your comment...hawana kipya. msemaji wa mwisho kesha maliza

    ReplyDelete
  2. Nakuona we Mazabali ni mtoto au juu kutupu. Yeye ni raisi wa nchi na ameajiriwa na wananchi. Yeye si nguvu pekee. Kuna mamilioni ya Watu, wasomi, wafanyakazi wengi wenye hekima kuliko mtu mmoja. Anajitambua kwa hili. Kuna sauti za Watu , bila hao yeye hana kazi?Kwa mwenendo, msimamo, na Kauli tunazozidi kuziona wakati mwingine ni aibu.Kiongozi anayetunishwa na sifa za nje ujue hajijui yuko wapi, kaajiliwa na nani, na anawatumikia nani, na analipwa na nani.Enzi za kikoloni, MADC wengi waliwanyanyasa Watanzania na kuwapiga viboko Watanzania kisa kusifiwa na manyapala wao ili kupewa Sukari. Inaonekana tunarudi huko. Nasifiwa na UN, Je Unasikia vilio vya kweli vya nchi hii, Watanzania wachapakazi bila maslahi wanashindwa kuwalisha watoto. Mtu wa UN anakusaidia nini?
    Hizi si kauli zinazotegemewa kutoka kwa Maraisi. Raisi nyerere aliwapa chao mabepari. Aliwalindanisha na chi ba simba. Si mtu wa kumkumbatia kama rafiki na kumchekea. Huyu si mtani wako kama Wazaramo la hasha. Hawa inabidi uwe serious wakuheshimu.Waheshimu nchi na Sheria za nchi. Wanakuja na mikataba yao jinsi wanavyoitaka nchi hii ikubali, badala ya nchi kuweka mgumu chini na kuwaambia hii ni Africa, Hii ni Tanzania, Ukitaka kuwekeza haoa ABCD. usipotaka Kwaheri. Ni nchi yetu na mali zetu. Weka wazi wote tuelewe .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad