Simba Yakimbilia TFF Baada ya Kutolizishwa na Waamuzi Katika Mchezo na Watani Wao wa Jadi

Simba Yakimbilia TFF  Baada ya Kutolizishwa na Waamuzi Katika Mchezo na Watani Wao wa Jadi

Klabu ya soka ya Simba imeandika barua ya kueleza malalamiko yake ya kutoridhishwa na maamuzi ya waamuzi katika michezo yake ya Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2017/18.

Hilo limebainishwa na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara wakati akiongea na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya klabu ambapo amesema nakala za barua hiyo wamezipeleka TFF, Bodi ya ligi TPLB pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
“Tumeliandikia barua shirikisho tukieleza dhuruma tunayofanyiwa na waamuzi pia nakala nyingine tumetuma kwa waziri mwenye dhamana ya michezo kwasababu haturidhishwi na maamuzi kwenye mechi zetu”, amesema Manara.
Manara ameeleza matukio mbalimbali ambayo klabu yake inalalamika kuhujumiwa ikiwemo Penalti mbili walizonyimwa dhidi ya Mbao FC ambapo mshambuliaji John Bocco alichezewa rafu lakini mwamuzi hakuchukua hatua sitahiki.

Matukio mengine ambayo Manara ameonesha kuchukizwa nayo ni kunyimwa Penalti kwenye mchezo dhidi ya Yanga Jumamosi iliyopita ambapo mlinzi Kelvin Yondani aliudaka mpira wa adhabu ndogo lakini mwamuzi Elly Saasi hakutoa adhabu ya Penalti.
Kwa upande mwingine Manara amesema klabu ya Simba inaendelea na maandalizi ya mchezo wake wa ligi dhidi ya Mbeya City chini ya kocha mkuu Joseph Omog na msaidizi wake Juma Masoud. Mchezo huo utapigwa siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad