Siri ya Rais Magufuli kumpa Angellah Kairuki Wizara ya Madini

Hizi inawezekana kabisa ndizo sababu kwanini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua na kumpa Angellah Kairuki Wizara mpya ya Madini.

1. Kutokana na kumudu vilivyo katika Ofisi aliekuwepo awali yaani Wizara -Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala bora.

2. Kutokana na Mh Kairuki kubuni mbinu mbalimbali za kuangalia upya mifumo ya ajira kwa kubuni uhakiki wa vyeti, uhakiki wa mifumo ya mishahara, ubunifu wa kupata taarifa za wafanyakazi halali na uhalali wa wafanyakazi waliopo na wale waliopo katika payroll yaani 'hewa' hali iliopelekea serikali kuokoa mabilioni ya shilingi.

Hiki ndicho kilichomsukuma kwa utashi na kwa imani alionayo kwa Mh Angellah Kairuki ndipo Mh Rais John Pombe Joseph Magufuli kumteua katika Wizara hii mpya ya Madini na Wizara ngumu iliowashinda wengi Ma- Dr na Ma- Professa hii itapelekea Angellah Kairuki ahakiki tena aina, na idadi ya migodi yote nchini kutokana na ubunifu na uaminifu alionao Mama huyu
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Piga kazi Angela

    ReplyDelete
  2. Wanawake ni wazuri sanaa katika maswala ya uongozi tena ni waminifu na wabunifu walio wengi. Angalau si wote

    ReplyDelete
  3. Huyu Dada Ni Mbunifu...!!!
    Ni Mchapa kazi...!!!
    Hodari na Msikivu...!!!

    Watanzania Tumuombee Mungu Asimbadilishe... Wizara ni Nyeti na ina Tempatation ya Kuiuza nchi kwa
    Economic HitMan's around the world.
    Imani Juu yake Tunayo na Atabadilisha Mtazamo na Mikataba yote kwa Maslahi ya Nchi yetu na Wananchi wetu.
    Magu hakufanya kosa katika Uteuzi wake wa Wizara yetu ambayo Mimi pia Nilikuwepo Huko Nyuma.
    Pls BeWare of Economi's hitman's ambao hutumia Tools kama World Bank/ Economica Infrastructure and the so Called Soft loans.
    Which end up into Huge Loans with hefty Interest and ends up buying you ( I'm sure you wont fall into this?)
    Nakuombe mungu akulinde na Tamaa na watakao kuzunguka wawe wanamuogopa mungu na Wazalendo wenye uadilifu tusiangukie kule kwa kina Ashanti wala Barrick na hawa middle (magumashi Acacia)
    Leo tumempa mzalendo mwenzetu kazi ngumu Pro Kabudi( Anaimudu) kwa hayo ya kina mwapachu na mlolongo wao.
    Mama Kairuki Mungu akulinde utulete maslahi nchi yetu.
    na kuibadilisha na kusitisha mikataba ambayo si ya win win situation kwa Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Kila mtu ajiombee mwenyewe akun kuombeana

    ReplyDelete
  5. Pambaneni na umaskini wenu wenyewe

    ReplyDelete
  6. Kutana na mtaalamu wa mitishamba anatibu ugumba ,uzaz .nguvu za kiume ,kukuza uume na kurefusha uume , kukuza hips shape na makalio ,maradh ya ini , uti sugu , mpigie dr 0744903557 tanga

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad