Sirro: Jeshi linatambua Makosa ya kimtandao yanayofanywa Mange Kimambi na linashughulikia

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro amesema jeshi lake linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwanadada Mange Kimambi na linashughulikia suala hilo .

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa IGP Sirro amesema jeshi hilo linatambua uvunjifu wa sheria ya makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwadada huyo maarufu mitandaoni ikiwemo kutoa machapisho mbalimbali ya matusi na kashfa kwa serikali na viongozi wake lakini kwa sasa hawezi kusema ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya mwadada huyo anayeishi nje ya nchi.

Aidha IGP. Sirro amesema Jeshi hilo halitawavumilia maafisa wa polisi na askari wanaowasaidia watu wanaofanya unyanyasaji kwa watoto kwa kuwafanyia vitendo vya ubakaji na ulawiti ili kukwepa mkono wa sheria huku akiwataka wananchi wanaohisi kutotendewa haki katika kushughulikia makosa ya aina hiyo kupeleke malalamiko kwa wakuu wa mikoa na viongozi wengine.

Chanzo: ITV channel
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama kweli huyo dada katenda kosa na ushahidi upo au kuna watu kawatendea makosa na yanakubalika kisheria ni makosa basi jeshi la police Tanzania linaweza kupeleka madai Interpol huyo dada akaamriwa kuja kujibu madai hayo. Au la sivyo afunguliwe faili lake la uchochezi faili limsubiri atakapokanyaga Tanzania mumshike. Kwa kweli saa nyengine huyo dada ni limbukeni sana kuwa Marekani anajiona kama yupo mbinguni. Kama walivyo baadhi ya watanzania wengine mbao kuwepo kwao nje ya nchi kuwa ni kichaka cha kujificha ili kuporomosha mitusi kwa viongizi wa nchi na kwa watanzania wengine. Mpinzani au mshabiki wa chadema akitukana ni demokrasia lakini akichukuliwa hatua kwa kuvuka redline ni udikteta? Basi kama ni udikteta na uwe udikteta lazima police mtimize wajibu wenu kuwashughulikia hawa vilaza.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad