Siwezi Kushindana na Flora Kulipiza Kisasi - Mbasha Afunguka

Msanii wa nyimbo za injili nchini Emmanuel Mbasha amefunguka na kusema katika maisha yake yeye anamuamini Mungu hivyo hawezi kuishi maisha kwa kushindana na aliyekuwa mkewe au kufanya jambo ili kulipa kisasi kwake.

Mbasha alisema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live akitambulisha video yake mpya 'Haleluyah' na kusema yeye hawezi kulipiza kuoa haraka kama ambavyo aliyekuwa mkewe alivyofanya.

 "Mimi ni mtu ambaye namuamini Mungu naishi maisha bila kulipiza na siwezi kulipiza kwani siishi kwa ajili ya kufanya mashindano, kama yeye alifanya akiamini kuwa yupo sawa na mimi siwezi kukurupuka kufanya hivyo ili watu wanione kuwa nimefanya hivyo, mimi nipo mwenyewe kama Mbasha ni ukweli ni kwamba sipo kwenye mahusiano yoyote kwa sasa" alisema Mbasha

Aidha Mbasha amesema kuwa waimbaji wengi wa nyimbo za injili ni watu ambao kweli wanamtumikia Mungu japo anakiri kuwa wapo watu wachache ambao ndiyo wamekuwa wakileta sifa mbaya kwa waimbaji wengine kutokana na matendo yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad