Mkazi mmoja wa kijiji cha Nyambale wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera ameilalamikia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kwa kushindwa kumkamata Mkuu wa Kituo cha Polisi Lusahunga anayedaiwa kuomba rushwa ya shilingi Milioni moja ili
aweze kuziachia ng'ombe 20 alizozikamata wakati zikipelekwa mnadani kwa madai kuwa hazikuwa na vibali vya kusafirishwa.
Akibainisha hayo mbele ya kamera za ITV Bi Bilatwa Mabuga katika kijiji cha Kibale na kusema kuwa tukio hilo limetokea wakati akisafirisha mifugo yake kutoka wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwenda kwenye mnada wa katoke wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitongoji cha Kabumbilo Bw. Paul Mussa aliyehusika kuwadhamini watuhumiwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Biharamulo Bi. Joyce Massi amelaani vikali unyanyasaji uliotokea.
Akijibu malalamiko hayo kwa masharti ya kutopigwa picha Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Biharamulo Bw.Hassan Mossi amekiri kupokea malalamiko ya mfugaji huyo