Kampuni kubwa ya simu za mkononi TECNO iliyopo chini ya TRANSSION HOLDINGS , imetambulisha rasmi simu yake mpya katika harakati zake za kukuza soko katika nchi za Asia na Africa, TECNO Phantom 8 katika jiji la Dubai.
Matumizi ya smartphone yanakua kwa kasi katika maeneo ya nchi za kiafrika na za mashariki ya kati kwa kiasi cha milioni 123. 7 mpaka 2016 toka milioni 106.4 mwaka 2015.
“Hivi karibuni ripoti zinaonyesha kwa kiasi kampuni imeweza kupenya katika soko na kuleta ushindani katika bara la Afrika na mashariki ya kati” Alisema makamu wa rais wa kampuni mama TRANSSION HOLDINGS, Arif Chowdhury. “Mipango yetu ni mwaka jana ilikua kukua zaidi kupitia mashariki ya kati hivyo kuzindua rasmi Phantom 8 jiijini Dubai ni hatua mojawapo katika kuendeleza mipango hii. Simu zetu zitaendelea kujikita katika kufuata mahitaji ya wateja zaidi”. Alimaliza Makamu wa raisi.
TECNO Mobile inaendelea kutoa bidhaa zenye ubora kwa wateja wake hasa barani Africa ambapo kampuni hiyo ina nafasi kubwa katika mauzo hasa kwa nchi kama Tanzania na Nigeria na nchi kadhaa kutokea mashariki ya kati.
Kwa zaidi ya miaka 11 TECNO imekua ikifanya kazi ya kuunganisha wananchi katika mawasiliano kupitia simu hasa kwa kuleta simu zenye ubora na bei inayoendana na watumiaji wake.
Simu hiyo iliyozinduliwa jijini Dubai imekua gumzo tangu tetesi zitoke kua inakuja sokoni imezinduliwa ikiwa na jina la Phantom 8 huku ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia kubwa hasa kwa upande wa kamera ikiwa na megapixel 20 mbele na kamera mbili nyuma6 GB RAM na ROM ikiwa ni 64GB. Kwa upande wa dizaini simu inametengenezwa vizuri ikiwa na muundo wa mithili ya Almasi na kioo.
Phantom 8 kutarajiwa kufika mabara mengine pia duniani.
Phantom 8 inauwezo wa kuweka “simcard” aina ya “Nano/ Micro” na inauwezo wa kumud memory card ya hadi 2TB (Terra Bytes) na pia inauwezo wa 4G plus ambayo inakuwezesha kutumia simu yako ndani na Zaidi ya nchi 200.
Kwa wateja waliopo Tanzania wataweza kuagiza simu hii mpya katika maduka maalumu ya simu za TECNO ili kuweza kuipata inapoingia sokoni siku chache zijazo.
Phantom 8 iliyozinduliwa hivi karibuni iikiwa imesheheni na sifa za kipekee kama Kamera, Ubo na muonekano wa kipekee pamoja na kasi ya ajabu. Kamera ikiw ana uwezo wa 20 MP, pamoja na kamera pacha zenye uwezo wa 13Mp +12 Mp kamera za nyuma ikiambatana na uwezo wa kuvuta picha mara 10 zaidi ya kamera ya kawaida, Ina uwezo wa HDR,4 in 1 uwezo wa kungarisha picha,AF na mambo mengine mengi yenye kukuhahkishia kupata picha zilizo bora na zenye muonekano mzuri.