Tunafanya Maandalizi kwa Wachezaji Wote Sijui Nani Atakayetuletea Point Tatu Katika Mechi Dhidi ya Yanga- Omog

Tunafanya Maandalizi kwa Wachezaji Wote Sijui Nani Atakayetuletea Point Tatu Katika Mechi Dhidi ya Yanga- Omog
ILI kupata ushindi ni lazima timu iandaliwe vizuri na si kutegemea mchezaji mmoja, hayo ni maneno ya Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, kuelekea mechi dhidi ya watani zao Yanga ambayo inatarajiwa kupigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 .
Omog aliliambia gazeti hili kuwa kikosi chake kinafanya mazoezi mara mbili kwa siku na mbali na mazoezi ya uwanjani, ameandaa pia darasa ambalo litakamilisha programu yake ya kuwavaa Yanga.

Mcameroon huyo alisema kuwa hakuna mechi nyepesi kwenye ligi au mashindano yoyote ya soka duniani, lakini mechi za watani zinakuwa na "presha" inayochangiwa na mashabiki na wanachama.

"Tunaendelea na maandalizi na yanahusisha wachezaji wote, hakuna mchezaji muhimu, siwezi kusema ninamtegemea nani katika mechi hiyo atakayetusaidia kupata pointi tatu, ili kushinda kila mmoja anatakiwa kutimiza majukumu yake, ninamatumaini tutafanya vyema, tuko kwenye nafasi nzuri," alisema Omog.

Naye mratibu wa timu hiyo, Abbas Ally, alisema kuwa kila mchezaji anafahamu "kiu" ya ubingwa ambao wanayo na ili kutimiza malengo hayo ni lazima wapate ushindi Jumamosi.

"Msimu uliopita tuliwafunga na mechi ya kwanza tulitoka sare, msimu huu tunahitaji pointi zote sita, tunaomba muda na saa itimie ili tuwaonyeshe kuwa huu ni mwaka wa Simba," Alisema Abbas.

Simba inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa kama ilivyo kwa watani zao, itakuwa na kocha mpya kwenye benchi lake la ufundi Mrundi, Masoud Djuma, ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Rayon Sports ya Rwanda aliyechukua mikoba ya Mganda, Jackson Mayanja.

Katika kujiandaa na mchezo huo, kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kimeweka kambi yake Unguja, Zanzibar wakati watani zao wanaofundishwa na Mzambia, George Lwandamina, wako Morogoro.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad